Impact Grant Fund
Kuhusu Impact Grant Fund (IGF)
Impact Grant Fund (IGF) ni mradi ulioanzishwa na Mfuko wa Kuendekeza Sekta ya Fedha Tanzania (FSDT) kwa ufadhili kutoka Umoja wa Ulaya (EU) chini ya Programu ya Huduma Jumuishi za Kifedha kwa ajili ya Ukuaji wa Biashara Ndogo na za Kati (MSMEs), Wanawake na Vijana (F4G). Kampuni ya KPMG Advisory Limited ndiyo inayosimamia utoaji wa mitaji ya mfuko huu.
IGF inalengo la kusaidia Biashara Ndogo na za Kati (MSMEs) zinazomilikiwa na kuendeshwa na wanawake na vijana zenye uwezo mkubwa wa kukua katika mikoa ya Morogoro, Manyara, Shinyanga, Rukwa, Kagera, Simiyu, Kigoma, Lindi, Mtwara, Singida na maeneo ya Mjini Magharibi, Zanzibar Kaskazini, Zanzibar Kusini, Pemba Kaskazini, na Pemba Kusini, huku ikizingatia zaidi biashara zinazomilikiwa na wanawake na vijana.
Kupitia mfuko huu, biashara zitakazokidhi vigezo zitaweza kupata mitaji yenye thamani ya hadi Shilingi milioni 30 za Tanzania, pamoja na msaada wa kukuza biashara. Mchanganyiko huu unalenga kuzisaidia biashara hizo kukua, kuboresha utendaji kazi, kufanya uvumbuzi, kutengeneza ajira na kujiandaa vyema zaidi kupata mikopo ya kibiashara.
Kwa ujumla, IGF inalenga kufungua fursa za ukuaji kwa biashara zenye tija huku ikichangia katika kujenga uchumi shirikishi na endelevu zaidi.
IGF imeanzishwa ili kuwezesha kutatua changamoto hizi na kutoa msukumo unaohitajika kwa biashara kukua, kupanuka, na kufikia fursa mpya za maendeleo.
Biashara ndogo na za kati zina mchango mkubwa katika uchumi wa tafaita, lakini bado zinakabiliwa na vikwazo vinavyozuia ukuaji wake, hususan:
- Ukosefu wa dhamana na changamoto ya kupata mikopo.
- Rekodi na mifumo dhaifu ya fedha.
- Kutazamwa na taasisi za fedha kama biashara zenye kiwango cha juu cha hatari katika kukopesheka.
- Upatikanaji mdogo wa huduma za fedha zinazokidhi mahitaji ya biashara.
Kupitia IGF, wafanyabiashara wadogo na wa kati watakaokidhi vigezo watawezeshwa:
- Kupata ruzuku isiyo rejeshwa kwa ajili ya kusaidia ukuaji wa biashara.
- Kuimarisha uwezo wa biashara ili kuboresha uendeshaji na usimamizi.
- Kuwekeza katika suluhisho zinazozingatia mabadiliko ya tabianchi na maendeleo endelevu.
- Kuboresha uwezo wa biashara kujiandaa kwa kupata ufadhili na kuongeza sifa zake za kuaminika kwa taasisi za fedha.
- Njia za kupata ufadhili wa ziada baada ya muda wa ruzuku.
Kupata huduma ya kuendeleza biashara, mafunzo ya kujiandaa kupata mikopo, pamoja na kuunganishwa na taasisi za fedha ili waweze kupata mikopo na ufadhili mwingine wa biashara katika hatua zinazofuata.
Impact Grant Fund (IGF) inatoa kipaumbele kwa biashara zinazofanya kazi katika sekta zinazochochea ukuaji
jumuishi, endelevu na unaostahimili athari za mabadiliko ya tabianchi, zikiwemo:
- Kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabianchi na kilimo mseto
- Uchumi mzunguko na utunzaji wa mazingira
- Uvuvi na ufugaji wa samaki endelevu, na uhifadhi wa rasilimali za bahari
- Urejeshaji wa bayoanuwai na mifumo ya kiikolojia
- Mnyororo baridi wa kuhifadhi na kusafirisha chakula
- Suluhisho bunifu na za kidijitali zinazowezesha kuhimili na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
- Nishati mbadala na teknolojia safi
Mfuko huu unalenga kuchochea ukuaji wa wafanyabiashara wadogo na wa kati, kwa ujumuishi wa watu wote, unaostahimili athari za mabadiliko ya tabianchi, na wenye matokeo endelevu kupitia maeneo matano muhimu:
- Ukuaji na Ubunifu wa Biashara: Kuwezesha biashara kupanuka, kuleta ubunifu, na kuimarisha mifumo yao ya uendeshaji.
- Utengenezaji wa Ajira na Ukuaji wa Kipato: Kuchochea fursa za ajira endelevu katika sekta mbalimbali.
- Uwezeshaji wa Wanawake na Vijana: Kuendeleza biashara zinazoongozwa na wanawake na vijana na kupunguza ukosefu wa usawa wa kimuundo.
- Kulinda Mazingira na Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi: Kuhamasisha biashara kutumia mbinu na teknolojia zinazolinda mazingira na kustahimili athari za mabadiliko ya tabianchi.
- Kuwezesha Upatikanaji wa Fedha: Kutumia ruzuku isiyorejeshwa kama kichocheo cha kuvutia mitaji na ufadhili zaidi kutoka sekta binafsi,
IGF inalenga biashara ndogo na za kati zenye uwezo mkubwa wa kukua Tanzania Bara na Zanzibar, hasa zile ambazo:
- Zinazolenga ukuaji na zinauwezo wa kukua na kujiendesha
- Zinaonyesha ubunifu na uwezo wa kuleta matokeo chanya katika jamii na kuboresha uchumi
- Zinamilikiwa, zinaongozwa, au zinawanufaisha wanawake na vijana
- Zinafanya kazi katika sekta zinazozingatia mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, au zinatumia mbinu hizo katika shughuli zao za biashara
Ili kukidi vigezo vya kupata ruzuku hii, waombaji wanapaswa kuwa na vitu vifuatavyo:
- Biashara ndogo, au ya kati iliyosajiliwa na inayofanya shughuli zake Tanzania Bara au Zanzibar.
- Biashara inayofanya vizuri, yenye uwezo wa kukua na kupanuka zaidi.
- Shughuli zinazojikita angalau sekta moja ya kipaumbele inayoungwa mkono na mfuko.
- Dhamira ya kuchangia utengenezaji ajira, hasa kwa vijana na wanawake.
- Kumilikiwa au kuongozwa na wanawake (angalau asilimia 51 ya umiliki) au vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 35.
- Kuonyesha uwezo wa kuchangia uhifadhi wa mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
- Kuwa tayari kushiriki katika mafunzo, ushauri na programu za kuimarisha uwezo wa biashara.
- Utayari wa kutumia ruzuku isiyo rejeshwa kwa ufanisi ili kukuza biashara.
- Uwezekano wa kupata mikopo au ufadhili mwingine wa biashara baada ya kupokea ruzuku.
Kipaumbele
Biashara zinazoongozwa na wanawake na vijana zitapewa kipaumbele katika mchakato wa uteuzi ili kuhakikisha makundi haya yanapata fursa zaidi za kushiriki na kunufaika na programu.
- Kutakuwa na awamu tatu za kupokea maombi ili kutoa fursa kwa biashara nyingi zaidi kushiriki na kuhakikisha maombi yanayowasilishwa
yanakuwa ya ubora wa hali ya juu. - Kila awamu ya maombi itakuwa wazi kwa muda wa wiki mbili, ili kuwapa waombaji muda wa kutosha kuwasilisha maombi yao.
Maombi yote yatapitia mchakato ufuatao:
- Yatawasilishwa kupitia mfumo wa maombi wa mtandaoni.
- Mwombaji atapokea uthibitisho wa kupokea ombi lake mara tu baada ya kuliwasilisha.
- Yatakaguliwa kwanza ili kuhakikisha taarifa na nyaraka zote muhimu zimewasilishwa na kwamba mwombaji anakidhi vigezo vya kustahili kabla ya kupelekwa katika hatua ya tathmini.
Kuchangia Vipaumbele vya Kitaifa na Kimataifa IGF inatekelezwa kuunga mkono malengo muhimu ya maendeleo ya kitaifa na kimataifa, ikiwemo:
- Awamu ya Tatu ya Mwongozo wa Kitaifa wa Ujumuishaji wa Huduma za Fedha (NFIF III)
- Mwongozo wa Kitaifa wa Fedha kwa Biashara Ndogo, Ndogo za Kati na za Kati (MSMEs)
- Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha (Financial Sector Master Plan).
Kwa kuwa ni mpango unaoungwa mkono na Umoja wa Ulaya (EU), IGF pia inachangia katika kufikia malengo
yafuatayo:
- Ukuaji wa uchumi unaowanufaisha watu wote kwa usawa.
- Ushirikishwaji na usawa wa fursa kwa wote.
- Hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuimarisha ustahimilivu.
Mafanikio ya IGF yatapimwa kupitia:
- Ukuaji na uendelevu wa biashara.
- Ongezeko la ajira.
- Ushirikishwaji wa makundi yenye fursa chache.
- Uwekezaji unaozingatia mazingira na kustahimili mabadiliko ya tabianchi.
- Upatikanaji wa mikopo na ufadhili mwingine baada ya msaada wa IGF.
Kwa maelezo zaidi kuhusu Impact Grant Fund (IGF) na Maswali Ya Mara kwa Mara (FAQs) Jusajili kupakua kipeperushi hapo chini.
About the Impact Grant Fund (IGF)
The Impact Grant Fund (IGF) is a financing initiative established by Financial Sector Deepening Tanzania (FSDT) with funding from the European Union (EU) under the Inclusive Finance for Growth of MSMEs, Women and Youth (F4G) Program. KPMG Advisory Limited is the Fund’s Grant Manager.
The IGF supports high-potential Micro, Small and Medium Enterprises (MSMEs) across Mainland Tanzania and Zanzibar, with a strong focus on women- and youth-owned businesses.
Through the Fund, selected MSMEs can receive non-reimbursable grants of up to TZS 30 million, together with business development support. This combination is intended to help enterprises grow, improve their operations, innovate, create jobs and become better prepared to access commercial financing.
Overall, the IGF aims to unlock the growth potential of promising MSMEs in Morogoro, Manyara, Shinyanga, Rukwa, Kagera, Simiyu, Kigoma, Lindi, Mtwara, Singida and Zanzibar Urban/West, Zanzibar North, Zanzibar Central/South, North Pemba, and South Pemba, while contributing to a more inclusive and sustainable economy.
MSMEs play a central role in Tanzania’s economy but continue to face constraints that limit their growth, particularly:
- Limited collateral and access to credit
- Weak financial records and systems
- Perceived high risk by financial institutions
- Limited access to appropriate financial products
IGF has been established as a catalytic financing instrument to address these constraints and unlock growth.
Through the IGF, selected MSMEs will receive:
- Grant financing to support business growth
- Capacity strengthening to improve operations and governance
- Support to invest in climate-smart and sustainable solutions
- Improved financial readiness and creditworthiness
- Pathways to access follow-on financing
- Selected enterprises will also receive business development support, credit readiness coaching, and introductions to financial service providers for follow-on credit
The IGF prioritises enterprises operating in sectors that drive inclusive, sustainable, and climate-resilient growth, including:
- Climate-smart agriculture and agroforestry
- Sustainable fisheries and aquaculture, and protection of marine resources
- Sustainable food cold chains
- Renewable energy and clean technologies
- Circular economy and waste management
- Biodiversity and ecosystem restoration
- Digital and innovative solutions supporting climate mitigation and adaptation
The IGF aims to catalyse inclusive, climate-resilient MSME growth through five key outcomes:
- MSME Growth and Innovation
- Supporting enterprise scaling, innovation, and formalisation.
- Job Creation and Income Growth
- Driving sustainable employment opportunities across sectors.
- Women and Youth Empowerment
- Advancing women- and youth-led enterprises and reducing structural inequalities.
- Climate and Environmental Impact
- Promoting environmentally sustainable and climate-smart business practices.
- Unlocking Finance
- Leveraging grants to crowd in private capital:
➡ At least 50% of supported MSMEs will access follow-on financing.
The IGF targets high-potential MSMEs in mainland Tanzania and Zanzibar, especially those that:
- Are growth-oriented and scalable
- Demonstrate innovation and impact potential
- Are led by or benefit women and youth
- Operate in or integrate climate-smart sectors
To be considered for support under the MSME Impact Grant Fund (IGF), applicants should:
- Be a registered MSME operating in mainland Tanzania and Zanzibar
- Demonstrate a viable, scalable business model with strong growth potential
- Operate within one or more of the priority thematic sectors
- Show commitment to job creation, particularly for youth and women
- Be owned or led by women (at least 51% ownership) or youth (aged between 18-35 years))
- Demonstrate potential to contribute to climate resilience and sustainability
- Be willing to participate in capacity strengthening support
- Demonstrate readiness to effectively utilise grant funding
- Show potential to access follow-on financing
Priority will be given to youth-led and women-led enterprises in line with programme inclusion targets.
IGF will adopt a three cycle call for applications approach to ensure broad participation and high-quality applications.
- A total of three calls for applications will be launched
- Application cycles will remain open for two weeks per cycle
All applications will be:
- Submitted through an online application platform
- Automatically acknowledged upon submission
- Subject to completeness and eligibility checks before review
The IGF is aligned with key frameworks, including:
- Tanzania’s National Financial Inclusion Framework III
- National MSME Financing Framework
- Financial Sector Master Plan
As an EU-supported initiative, it also contributes to:
- Inclusive and equitable economic growth
- Diversity and social inclusion
- Climate action and resilience
Success will be determined by:
- Enterprise growth and sustainability
- Job creation outcomes
- Inclusion of underserved groups
- Climate-resilient investments
- Access to follow-on financing
For more information about the Impact Grant Fund (IGF) and Frequently Asked Questions (FAQs), register below to download the brochure.