FSDT-Logo-white

FSDT yazindua kampeni ya ‘BIMA CHALLENGE’ nchini Tanzania

bimaLeo tarehe 28 Juni 2016 Dar es Salaam, Tanzania- Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania (FSDT), umezindua kampeni shindanishi ya kuwezesha bima kwa watu wa kipato cha chini, kupitia mfuko wa fedha uitwao ‘Bima Challenge’ kwa lengo la kuchochea maendeleo ya sekta ya Bima kwa watu wa kipato cha chini Tanzania, inayokusudia kuwajumuisha watu wa kipato cha chini kwenye mfumo wa bima.

Kampeni hii ya miezi 12, iliyozinduliwa leo katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro ni ya kwanza na ya aina yake hapa nchini. Lengo kuu la kampeni hii ni kuchochea maendeleo ya huduma ya bima shirikishi Tanzania. Hii ni pamoja na kukuza soko la bima nchini Tanzania kupitia uwezeshaji wa kifedha, kusaidia ubunifu wa bidhaa, majaribio ya bidhaa hizo na kuboresha huduma kwa wateja wa bima ili kuwa katika kiwango kinachotakiwa na urahisi wa upatikanaji wake kwa watu wa kipato cha kawaida nchini.

Kwa muujibu wa utafiti uliofanywa na FSDT, Sekta ya bima nchini Tanzania bado haijaweza kuwafikia watu wengi nchini na hata wamiliki na waendeshaji wa sekta hiyo wamekuwa na mawazo yanayofanana katika uendeshaji wake. Hivyo basi ‘Bima Challenge’ inatoa changamoto na pia fursa ili kuwahamasisha wadau mbalimbali kuja na mawazo au fikra mbadala ambazo zitawezesha kuibadilisha sekta ya bima ili iweze kufanyika kwa ufanisi zaidi nchini Tanzania.

“Kuna upungufu mkubwa wa huduma ya bima kwa watu wa kipato cha chini katika Tanzania na ni matumaini yetu kwamba Bima Challenge itakuwa suluhisho kwa kuchoche ubunifu wa bidhaa mpya zitakazokuwa na tija kwa maisha ya mwananchi wa kawaida, familia na wajasiriamali ambao kwa sasa wanakosa huduma hii,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa FSDT, Bwana Sosthenes Kewe.

Akifafanua namna wadau wa bima wanavyoweza kushiriki katika kampeni hii, Mkuu wa Kitengo cha Bima FSDT, Bi. Kemibaro Omuteku alisema watu wanaopenda kushiriki ni lazima washirikiane na makampuni ya bima ili kutumia taratibu za bima katika utoaji wa huduma hizo mpya zitakazobuniwa.

Iwapo mtu, au kampuni husika ikiwa na wazo la kiubunifu ambalo wanaamini litaonyesha utofauti wa namna ya kuendesha sekta ya bima, watajaza fomu za kushiriki kupitia mtandao wetu. ” Alisema. Tumeonyesha hatua muhimu ambazo zinapaswa kufuatwa kwa umakini zinazobainisha mtu mwenye sifa. Licha ya hatua hizo pia tuna jopo la wataalamu ambao wanapitia maombi yaliyotumwa, kuhakikisha kwamba kila mmoja anapata nafasi ya ushiriki kwa haki,” aliongeza.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Uendelezaji wa Bima kwa Watu wa Kipato cha Chini (TWG), Bwana Julius Magabe alisema Bima Challenge ni nafasi ya kuleta mabadiliko katika sekta ya bima kwani itafungua fursa kwa makampuni na wateja kunufaika. Alibainisha kwamba hatua hiyo itaimarisha ukuaji wa soko, itaimarisha ubora wa bidhaa zinazotolewa na kuleta ufanisi kwa wateja ikiwamo kujenga uwezo katika usambazaji na kupokea bidhaa.

“Kwa mara ya kwanza kama makampuni ya bima tumepewa nafasi kuwekeza katika maeneo mapya kwetu ikiwamo kupunguza gharama za uwekezaji, utafiti na changamoto’ aliongeza.

“Natumia fursa hii kuipongeza FSDT kwa kuanzisha kampeni hii ya kiubunifu yenye lengo la kuimarisha sekta ya bima na ujasiriamali nchini,” alihitimisha.

***Mwisho.***

KUHUSU SHIRIKA LA FSDT

Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania (FSDT) ni taasisi ambayo ilianzishwa mwaka 2004 ikiwa na lengo la kuimarisha mfumo wa soko ambao unawanufaisha watu, kaya na wajasiriamali kwa kuwajengea uwezo na kuwapa fursa ili kuboresha maisha yao. Hii inajumuisha kubainisha changamoto na kusaidia ubunifu na kujenga uhusiano katika sekta ya fedha kupitia ushirikiano wa wadau mbalimbali katika sekta hiyo.

Kwa taarifa zaidi kuhusu FSDT, tafadhali tembelea; www.fsdt.or.tz

Kwa mawasiliano
Neema Mosha
neema@fsdt.or.tz

KUHUSU TAASISI YA TECHNICAL WORKING GROUP (TWG)

The Microinsurance Technical Working Group(TWG) ni Taasisi au chombo cha serikali kilichoundwa tangu mwaka 2013 kikiwa na lengo la kuendesha mpango wa utekelezaji wa maendeleo ya sekta ya bima kwa watu wa kipato cha chini.

Mkakati wa TWG unalenga hasa katika kuchochea mahitaji , uimarishaji wa ugavi na uwezeshaji wa mazingira mazuri ili kuiwezesha sekta ya bima kupatikana kwa urahisi nchini.

Kwa habari zaidi kuhusu TWG wasiliana na:
Richard Sentongo
Richard.sentongo@gmail.com

Facebook
Twitter
LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *